Malengo ya timu ya Wanajangwani ni kufika nusu fainali ya klabu bingwa barani Afrika na safari yao itaanza kesho dhidi ya Al-Hilal S.C ambayo si timu nyepesi kutokana na historia ya timu hiyo katika mashindano ya vilabu ya CAF.Yanga SC itaingia kwenye mchezo huu ikikumbuka msimu wa 2021-2022 ambapo iliondoshwa kwenye mashindano ya klabu bingwa dhidi ya mpinzani wake wa kesho.
Nafasi ya Ukurugenzi wa ufundi ni nafasi nyeti sana kwenye timu kwani mipango ya timu kuanzia falsafa ya timu aina ya uchezaji wa timu Wachezaji wanaohitajika na timu kulingana na aina ya falsafa iliyopo kwa wakati huo, mipango ya baadae aina gani ya Kocha aajiriwe yote ipo chini ya utendaji wa Mkurugenzi wa ufundi.
Carsley alichukuwa nafasi ya aliyekuwa Kocha wa timu hiyo Gareth Southgate aliyejiuzulu baada ya michuano ya UEFA Euro 2024. Ameiongoza timu hiyo michezo sita akifanikiwa kushinda michezo mitano na kupoteza mmoja dhidi ya Ugiriki uliofanyika mwezi Oktoba 2024.
Stars inahitaji matokeo ya ushindi kama inahitaji kufuzu kwa mara ya tatu mfululizo mashindano hayo baada ya kufanya hivyo 2019,2023 inayosubiriwa kuona tutapata matokeo ya ushindi dhidi ya Guinea, Tanzania itakuwa imejihakikishia kufuzu AFCON kwa mara ya nne katika historia yake 1980,2019,2023 na 2025.
Nyota huyo wa zamani wa VfL Wolfsburg na Borussia Mönchengladbach anatarajiwa kufanya makubwa kikosi cha Yanga FC kutokana na kurithi kikosi chenya Wachezaji bora walio washindani.Kazi yake ya kwanza itakuwa kurudisha viwango vya Wachezaji vilivyoporomoka, pili kusimamia nidhamu za Wachezaji wa kikosi hiko kutokana na kuvuja kwa taarifa kuhusiana na nyota wengi wa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu Tanzania bara kuendekeza starehe na kuporomosha viwango vyao.
Miguel Gamondi alijiunga na Yanga SC Juni 2023 kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mwalimu wa timu hiyo ya Wananchi Mtunisia Nesreddine Nabi ambaye alitimkia AS FAR Rabat ya nchini Morocco.Gamondi anayesifika kwa uwezo wake mkubwa wa kufundisha mpira wa kushambulia na burudani kutokana na asili yake ya America ya Kusini kucheza mpira huku ukiwa na tabasamu mdomoni mwako.Ameiongoza timu ya Wanajangwani kushinda Kombe la Shirikisho Tanzania, Kombe la Ligi kuu Tanzania bara pamoja na kucheza hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika.
Kali Ongala ni Kocha mwenye uzoefu aliyewahi kufundisha timu ya Azam FC na timu za vijana za Tanzania.Pia amewahi kucheza klabu ya Yanga siku za nyuma uzoefu wake wa kucheza mpira pamoja na kufundisha Tanzania unaweza kuisaidia kwa kiasi kikubwa KMC kuyafikia malengo yake ya msimu huu wa 2024-2025.
Nyota huyo wa Hispania mwenye umri wa miaka 22 amekuwa muhanga wa majeraha ya mara kwa mara hivyo kufifisha kiwango chake cha uchezaji alichokionyesha akiwa na umri wa miaka 16 wakati anapandishwa kucheza kikosi cha kwanza cha Barcelona. Fati alitabiriwa makubwa ndani ya Catalunya mpaka kupewa jezi namba 10 iliyovaliwa na nyota kama Ronaldinho Gaucho na Lionel Messi ambaye alihamia PSG ya Ufaransa.
Stars inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi H ikiwa na alama zake 4 baada ya kucheza michezo minne ikishinda mechi moja ikitoka suluhu mechi moja na kupoteza michezo miwili mfululizo dhidi ya timu ya taifa ya Congo DRC.
Leroy Sane Winga wa kimataifa wa Ujerumani na klabu ya Bayern Munich.
Moalin alijiunga na KMC FC kutokea Azam FC alikofukuzwa kazi Augosti 29 2022.Raia huyo wa Marekani alitoa sababu tano zilizomfanya kuondoka KMC FC ikiwa bado mapema mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara kutokana na kushindwa kuvumilia mazingira ya kazi kwenye kikosi hiko.
Malacia amekaa nje ya uwanja tangu aitumikie timu ya taifa ya Uholanzi dhidi ya Crotia mchezo wa mashindano ya ligi ya mataifa ya bara la Ulaya uliofanyika mwaka 2023.Baada ya hapo Mchezaji huyo amekuwa muhanga wa matatizo ya goti yanayomsumbua mara kwa mara kurejea kwake uwanjani mwezi Februari kuliahirishwa kutokana na kuhofia kumuharakisha kurudi uwanjani na kutonesha jeraha lake.
Mchezaji huyo kaitumikia timu yake michezo 16 mchezo wake wa mwisho ukiwa Oktoba 6 siku moja kabla ya kupata ajali ya gari akiwa na Rafiki zake.Kaitumikia michezo 3 timu yake ya taifa mchezo wake wa kwanza ukiwa ule wa Novemba 22 dhidi ya Iraq ambao ulitamatika kwa suluhu ya kutokufungana.
Huu ni mwanzo bora wa ligi ya kikapu Marekani NBA tangu msimu wa 2015-16 klabu ya Golden State Warriors iliyocheza michezo 24 mfululizo kwenye msimu huo.Donovan Mitchell amekuwa kwenye kiwango bora sana msimu kwa Cavaliers kamaliza mchezo wa jana akiwa amefunga alama 36 na Wachezaji wengine watano wamefikisha alama zaidi ya kumi mchezo wa jana huku ikitoka nyuma kwa alama 9 robo ya tatu na kushinda mchezo huo.
Sababu mbalimbali zimetajwa juu ya uamuzi uliochukuliwa na Uongozi wa timu hiyo kuhamia uwanja wa KMC Complex ikiwemo picha za vidio ambazo hazina uthibitisho kama kweli zinaihusu klabu hiyo zikionyesha mabomba ya sindano uwanjani Azam Complex ikisemekana Wachezaji wake wanaongeza nguvu kwa kuchoma sindano.