
TETESI ZA SOKA AFRIKA
Kocha wa Al Ahly Jose Riveiro ameripotiwa kuufahamisha uongozi wa klabu hiyo kuhusu kuboreshwa safu ya ulinzi akiwemo beki ya kushoto, beki wa kulia na beki wa kati. Riveiro anatajwa kuhitaji huduma ya beki wa kulia wa Ceramica Cleopatra, Ahmed Hany mwenye umri wa miaka 28.
Klabu ya APR FC imetangaza kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Uganda, Ronald Ssekiganda!
Hussein Kazi amejiunga na kikosi cha Namungo kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Simba SC.
Kocha wa zamani wa Wydad Casablanca na Mamelodi Sundowns Rulani Mokwena anadaiwa kukataa ofa tatu kutoka kwa wababe wa Misri Pyramids FC, klabu ya Saudi Arabia Al Jandal SC, na klabu ya Qatar Al Shahaniya huku ikitajwa kuwa anaweza kujiunga na MC Algiers kwa msimu wa 2025/26 baada ya kuondoka kwa Khaled Ben Yahia.