Jumatatu , 23rd Feb , 2026

Msanii maarufu wa hip hop, Young Thug, amefichua rasmi jina la albamu yake ijayo itakayojulikana kama “DBC”. Tangazo hilo amelitoa kupitia mtandao wa kijamii wa X, baada ya awali kuwapa mashabiki dokezo kupitia Instagram.

Young Thug, anayejulikana pia kwa jina la Thugger, amekuwa kimya kimuziki kwa kipindi fulani, jambo lililoongeza hamasa miongoni mwa mashabiki wake wanaosubiri kwa hamu kazi mpya.

 

Mpaka sasa, bado hajatangaza tarehe rasmi ya kuachia albamu hiyo, lakini taarifa ya jina pekee tayari imezua mjadala mkubwa mtandaoni, huku mashabiki wengi wakionesha shauku yao ya kusikia muziki mpya kutoka kwake.