Jumanne , 29th Sep , 2015

Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imesema kuwa imejipanga vizuri kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapiga kura bila bugudha yoyote kwa kuwaandali mazingira rafiki.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) Jaji Damian Lubuva.

Akizungumza katika mkutano na watu wenye ulemavu Mwenyekiti wa NEC Jaji Damian Lubuva amesema kuwa wameandaa karatasi maalumu kwa ajili ya watu wasioona ili kuwapa fursa ya kumchagua kiongozi wanayemta kwa hurahisi.

Jaji Lubuva ameongeza kuwa mpaka sasa idadi ya waliojiandikisha kupiga kura ni watu millioni 23.7 japo Uchakatuaji wa majina ya watu katika daftari la wapiga kura kwa mfumo wa BVR unaendelea na zoezi likimalizika Tume itatoa idadi ya mwisho ya watu watakaopiga kura oktoba 25 mwaka huu.

Wakati huo huo Lubuva amevionya vyama vya siasa kufanya kampeni za kistaarabu na Tume itamchukulia hatua kali mgombea atakayetumia lugha za kejeli na kuwataka kunadi sera zao na kuacha kuzungumzia watu.