Alhamisi , 5th Feb , 2026

Utafiti wa muda mrefu uliochapishwa kwenye jarida la ''The Journals of Gerontology'' nchini Marekani, umebaini kuwa wanaume waliooa wanawake wenye elimu kubwa wana uwezekano mkubwa wa kuwa na afya bora ya ubongo wanapozeeka.

Watafiti wanasema kuwa na mwenza "Mwenye akili" husaidia akili ya Mwanaume kutanuka kila siku kupitia Mazungumzo ya kina (Deep conversations) na kufanya matatizo ya maisha kuwa rahisi kuyatatua kwa pamoja.

Hata kama Mwanaume hana Elimu kubwa sana, kuishi na mwanamke msomi kunamsaidia kuondokana na ugonjwa wa kusahau kwa asilimia kubwa atakapokuwa Mzee.