Jumanne , 3rd Feb , 2026

Mwaka 2011, LeBron James alifanya uwekezaji kwa kununua 2% ya hisa za klabu ya Liverpool kwa thamani ya Dola Milioni 6.5 (takriban TSh Bilioni 16.7) wakati huo, klabu nzima ilikuwa na thamani ya Dola Milioni 325 tu.

 

Leo hii, thamani ya Liverpool imepanda hadi kufikia Dola Bilioni 4.8 (takribani TSh Trilioni 12.3) Hii inamaanisha kuwa zile hisa za LeBron zimepanda thamani kutoka Milioni 6.5 hadi kufikia Dola Milioni 96, Kwa Shilingi ya Tanzania ni takriban Bilioni 247.6 

Uwekezaji wa LeBron umeongezeka mara 15 zaidi ya kiasi alichoweka awali, na akiwa mwanahisa pia wa Kampuni Mama ya FSG inayomiliki karibu asilimia 80 ya Klabu hiyo.