Alhamisi , 29th Oct , 2015

Licha ya mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha kutangaza kufutilia mbali kwa matokeo ya uchaguzi visiwani humo,Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetoa tamko kuwa hatua hiyo haitaathiri matokeo ya uchaguzi wa urais Tanzania bara.

MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva,

Kupitia kwa taarifa iliyoitoa kwa vyombo vya habari mwenyekiti wa NEC jaji mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa mchakato wa uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utaendelea kama kawaida.

Jaji Lbuva amesema kuwa uchaguzi wa Rais na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaosimamiwa na tume ya taifa ya uchaguzi ni tofauti na uchaguzi wa serikali ya mapinduzi Zanzibar.

Aidha mwenyekiti huyo amesema hadi sasa tume imeshapokea matokeo ya kura za Rais kutoka majimbo yote ya Zanzibar na imeshayatangaza na hakuna kasoro yoyote iliyotolewa katika mchakato huo.