Jumanne , 17th Feb , 2026

Rapa na muimbaji wa kike Marekani Coi Leray amembwambia Boyfriend wake Justin Laboy kuwa mwanaume ku-like picha za wanawake wengine mitandaoni ni usaliti.

Coi Leray na mpenzi wake Justin Laboy

Coi Leray amesema hilo akizungumzia na Justin Laboy kupitia Podcast yake ya "Respectfully, "The Justin Laboy Show".

"Ku-like picha ni usaliti siamini kama kuna bahati mbaya" anasema Coi Leray

Pia ameongeza kusema wanaume walio kwenye mahusiano hawatakiwi kuwa na marafiki wa kike.

Japo mpenzi wake alipinga mtazamo huo wa ku-like picha za wanawake wengine ni usaliti sababu anaweza kukutana na picha hizo kwa bahati mbaya na ku like bila kujua.