Alhamisi , 17th Aug , 2023

Kampuni ya simu za mkononi nchini ya Vodacom imezindua kampeni mahususi ambayo inalenga wananchi wengi wa Tanzania kuweza kujipatia mikopo ya simu janja kampeni ambayo imepewa jina la miliki simu lipa mdogo mdogo

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo iliyoshirikisha pia benki ya NMB pamoja na Mtandao wa Google Mkurugenzi wa Fedha wa Vodacom Tanzania Hilda Bujiku amesema kampeni hiyo inakwenda kumgusa mwananchi wa kawaida ambaye huenda amekuwa hawezi kununua simu za smartphone ama simu janja na badala yake amekuwa akitumia kitochi

 "Dunia kwa sasa inakwenda na mabadiliko ya teknolojia hivyo kila Mwananchi haijalishi ni WA Hali gani anapaswa kumiliki simu hizi ili aweze kuendana na teknolojia ya sasa'' Amesema Hilda Bujiku Mkurugenzi wa Fedha Vodacom Tanzania

Kwa upande wake Filbert Mponzi ambaye ni Afisa mkuu wa wateja binafsi na biashara benki ya NMB amesema wanatambua kwamba serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Dk Samia Suluhu Hassan imekuwa ikisisitiza zaidi wananchi kwenda kidigitali hivyo kampeni hiyo inalenga kuunga mkono jitihada hizo 

"" Sisi kama NMB benki na Vodacom pamoja na Mtandao huu wa Google malengo yetu ni kuhakikisha teknolojia hapa nchini inakua kupitia kwenye mitandao ya simu'' Amesema Filbert Mponzi Afisa mkuu wa wateja binafsi na biashara NMB benki

Naye George Lugata ambaye ni meneja mauzo'' na usambazaji Vodacom Tanzania ameeleza namna ya kupata simu hizo ikiwemo vigezo ambavyo vimezingatiwa Ili Mwananchi aweze kupata simu hizo za mkopo katika madukanya Vodacom

"" Kigezo kimojawapo ni pamoja na kuwa mteja wa Vodacom lakini ingawa mtu ambaye sio mteja anaweza kununua moja kwa moja'' Amesema George Lugata meneja wa mauzo'' na usambazaji Vodacom Tanzania