Jumatatu , 14th Mar , 2016

Hospitali ya Mwananyamala ya Jijini Dar es Salaam ipo mbioni kupata ahueni ya kupunguza foleni ya wagonjwa wanaohitaji kufanyiwa upasuaji baada ya wafadhili kujitokeza kujenga majengo ambayo yatatumika kwa ajili ya Upasuaji.

Jengo la Wazazi Hospitali ya Mwananyamala

Jengo hilo litakalokua na vyumba sita ambapo vyumba viwili vitakua vya upasuaji, viwili vitakua vya kupumzikia na viwili kwa wagonjwa mahututi ikiwa ni msaada kutoka shirika la kimaendeleo la kitanzania la GSM.

Wakiongea wakati wa uzunduzi wa Ujenzi huo wakina mama hospitalini hapo wamesema itakua ni mkombozi wa kuepusha vifo vya kina mama wajawazito ambao wengi wao walikuwa wanafariki njiani wakati wakihamishiwa hospitali nyingine zenye huduma hiyo.

Aidha wamesema kuwa hospitali hiyo kubwa ambao inategemea na wakazi wengi wa manispaa ya Kinondoni na Wilaya jirani itaweza kupunguza msongamano katika hospitali ya taifa ya muhimbili ambapo kina mama wengi hukimbilia huko kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji.