
Jamie Carraghe na Cole Palmer
'Nikiwatizama Chelsea, nafikiri walichofanya kwenye Kombe la Dunia la Vilabu, kila timu ilitamani kushinda. Real Madrid, PSG na Manchester City wote walitamani kushinda, na hizo ndio timu ambazo tuliamini bora zaidi. Kitendo cha The Blues kushinda taji nadhani itasaidia kujenga uhusiano kati ya Enzo Maresca na mashabiki, ambao ulikosekana msimu uliopita.
''Sina uhakika kama Maresca ataisukuma Chelsea kuwania ubingwa. Chelsea inafanya sana biashara, katika miaka michache iliyopita, timu imekuwa na mabadiliko ya kikosi kuingia na kutoka wachezaji wengi pasipo kuwa na mtu sahihi wa kupandisha kiwango cha timu. Cole Palmer amekuwa na kiwango bora, lakini mawinga wao wote hawaendani uwezo, Mfano mzuri ni Gittens ameingia nafasi ya Madueke, hakuna utofauti hapo, na ninaona hilo kwenye nafasi nyingi tu.''
Chelsea tayari imeachana na Wachezaji wenye majina makubwa msimu huu wa joto, akiwemo Joao Felix, Kepa Arrizabalaga na Kiernan Dewsbury-Hall wameondoka kwa mikataba yenye thamani ya zaidi ya £150m kwa pamoja.
Maingizo mapya ni Joao Pedro (£60m), Liam Delap (£30m), Jorrel Hato (£37m), Estevao Willian (£28m), Dário Essugo (£18.5m), na Mamadou Sarr (£12m) pamoja na winga wa England chini ya umri wa miaka 21 Gittens kutoka Borussia Dortmund aliyejiunga kwa pauni milioni 55.