Ijumaa , 6th Mar , 2026

Baada ya Shirikisho la Soka la Morocco kumtangaza Mohamed Ouahbi (Wahbi) kuwa Kocha mkuu wa timu ya timu Taifa ya Soka ya Wanaume "The Atlas''  akichukua nafasi ya Walid Regragui aliyetangaza kuachia ngazi hapo jana Machi 05/2026, Wahbi amepewe jukumu la kuifikisha Morocco mbali kisoka

Mohamed Ouahbi (Wahbi)

Malengo makuu aliyopewa Mohamed Ouahbi (Wahbi) baada ya uteuzi wake ni kufanya vizuri kwenye Kombe la Dunia 2026 ambapo Morocco itashiriki ikiwa kwenye kundi C pamoja na Brazil, Scotland na Haiti. Ouahbi anatakiwa kuendeleza mafanikio ya Morocco baada ya kufika nusu fainali ya Kombe la Dunia 2022 na kuhakikisha timu inafanya vizuri tena.

Aidha Morocco wanaamini kuwa Wahbi  ataleta maono mapya na nguvu mpya kwenye timu pamoja na kuendeleza kizazi kipya cha wachezaji kutokana na sifa yake ya kukuza vipaji vya vijana, na aliiongoza Morocco kushinda FIFA U-20 World Cup 2025 dhidi ya Argentina.

Hivyo anatarajiwa kuunganisha wachezaji vijana na wakongwe ili kujenga timu ya muda mrefu na kudumisha hadhi ya Morocco kama moja ya timu bora barani Afrika na duniani baada ya mafanikio ya miaka ya hivi karibuni.