Jumatatu , 2nd Mar , 2026

Mahakama nchini Romania imeripotiwa kukataa rufaa ya rapper Wiz Khalifa dhidi ya hukumu yake ya miezi tisa jela kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya (Bangi).

Kwa mujibu wa Mahakama ya Rufaa huko nchini Romania ilitoa uamuzi huo Februari 26 ikiwa ni mwezi mmoja baada ya msanii huyo kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.

Sakata hilo linatokana na tukio la Julai 2024, ambapo polisi wa Romania walimkamata #WizKhalifa kwa tuhuma za kuvuta bangi jukwaani wakati wa tamasha lililofanyika nchini humo.

Mamlaka zilisema kuwa Wiz Khalifa alikutwa na gramu 18 za bangi, jambo ambalo ni kinyume cha sheria  za Romania kuhusu matumizi na umiliki wa bangi.

Mara ya kwanza Wiz Khalifa alipigwa faini na baadaye waendesha mashtaka walikata rufaa wakitaka adhabu kali zaidi Rufaa hiyo ilikubaliwa Desemba mwaka jana, na kusababisha kutolewa kwa hukumu ya kifungo cha miezi tisa jela.

Bado haijulikani kama mamlaka za Romania zitachukua hatua za kumrejesha msanii huyo nchini humo ili akatumikie kifungo hicho.