Ijumaa , 6th Mar , 2026

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam leo, Ijumaa Machi 06.2026 imesikiliza maombi yanayotokana na shauri la madai Na.8323/2025, maombi yaliyoletwa Mahakamani hapo na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Tundu Lissu.

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam leo, Ijumaa Machi 06.2026 imesikiliza maombi yanayotokana na shauri la madai Na.8323/2025, maombi yaliyoletwa Mahakamani hapo na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Tundu Lissu.

 Shauri hilo lililoanza majira ya saa tatu saa za Afrika Mashariki, lilianza kwa Wajibu maombi ambao ni wadaaiwa wote walioko kwenye shauri la madai Na. 8323/2025 linalohusu usawa kwenye mgawanyo wa mali kati ya Tanzania Bara na Zanzibar ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao ni Saidi Issa Mohamed, Maulidah Anna Komu na Ahmed Rashid Khamis ambao ni waleta maombi kwenye shauri hilo la msingi.

 Sambamba na hao pia wapo Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa Chama hicho John Mnyika ambao kimsingi ni wajibu maombi kwenye shauri la msingi, linalosikilizwa mbele ya Jaji Hamidu Mwanga .

 Akizungumza mbele ya Jaji Mwanga, Lissu amesema maombi hayo yameletwa kwa njia ya hati ya maombi yaani (‘’Chamber Summons’’) huku  ikiungwa mkono na hati ya kiapo chake ya Desemba 12.2025.

Ameanza kwa kuzungumzia msingi wa kisheria wa maombi hayo ambapo amesema, hati ya maombi inaonesha wazi kuwa maombi hayo yameletwa chini ya masharti ya amri ya kwanza ya kanuni ya 10 kifungu kidogo cha (2) ya sheria ya mwenendo wa madai, sura ya 33 ya sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika kesi hiyo,bado walalamikaji ambao walalamikaji wanasema wadaiwa wamekiuka kifungu cha 6A (1), (2), (5) cha Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 258 Marejeo ya mwaka 2019 na iwaelekeze wazingatie kifungu hicho ili wawe sehemu ya mali.

Baadas ya kusikiliza pande zote mbili,jaji anayesilikiliza shuri hilo Hamidu Mwanga ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 26 ambapo atakuja kutolea uamzi rasmi wa Tundu Lissu kushirki katika katika kesi hiyo au lah!

Ikumbukwe kuwa Tundu Lissu alifungua maombi hayo mnamo Novemba 14, 2025 akiomba kujumuishwa katika shauri hilo kama sehemu ya wajibu maombi.