Jumamosi , 15th Nov , 2014

Kundi mahiri la muziki Ruby Band, baada ya kuanza kujizolea mashabiki kwa kasi kupitia ngoma ya Kisebusebu ft Hans Waleo, limejinadi kuleta ladha ya tofauti katika uimbaji na vilevile maonesho katika tasnia ya Bongo Flava.

Ruby Band

Kundi hili linaloundwa na Sumalay, Maya, Kwea Pipa na C Minor chini ya Madam Ruby katika story na eNewz, pia wamefafanua maana ya ngoma ya Kisebusebu na vilevile kuahidi ladha kali zaidi kuanzia mwaka ujao.

Wakiongea kwa pamoja na eNewz, Bendi hii imewaahidi mashabiki wake kazi mpya kali kuanzia mwezi wa kwanza mwaka ujao huku wakifunga mwaka vizuri kabisa na Kisebusebu.