Ijumaa , 8th Mei , 2026

Uongozi wa Klabu ya Real Madrid imetangaza kuwaadhibu wachezaji wao Federico Valverde na Aurélien Tchouaméni baada ya ugomvi kati yao uliopelekea Valverde kupelekwa hospitali. Taarifa ya Klabu inaesema;

Federico Valverde na Aurélien Tchouaméni

"Kufuatia matukio yaliyosababisha kesi za kinidhamu zilizoanzishwa jana dhidi ya wachezaji Federico Valverde na Aurélien Tchouaméni, wote wawili walijitokeza leo mbele ya mpelelezi aliyepewa jukumu la kesi hiyo.

"Wachezaji hao walielezea majuto yao kamili kwa kile kilichotokea na kuombana msamaha. Pia waliomba msamaha kwa klabu, wachezaji wenzao, makocha, na mashabiki, na wote wawili wamejitolea kwa Real Madrid kukubali adhabu yoyote ambayo klabu inaona inafaa".

"Baada ya kuomba msamaha Real Madrid imeamua kuweka adhabu ya kifedha ya Euro laki tano (bilioni 1.5 Tsh) kwa kila mchezaji, na hivyo kuhitimisha taratibu zinazolingana za ndani"