Ijumaa , 10th Jul , 2026

 Kwenye Podcast ya ‘The Joe Rogan Experience’ mwaka 2020 Kanye West alitoa mtazamo wake wa namna gani mfumo wa maisha umetengenezwa kwa ajili ya watu wachache.

Kanye West amesema pesa si suluhisho la kila kitu, bali ni mfumo ulioundwa na binadamu na watu wameaminishwa kuufuata.

Kanye West anasema, “Kama pesa ndiyo jibu la matatizo yote, kwa nini zisichapishwe nyingi ili kila mtu apate?”

Pia ameufananisha mfumo wa sasa na Dola ya Roma na meli ya Titanic, akidai unawalinda wachache wenye nguvu huku ukiwafanya wengi waendelee kuamini kuwa utajiri na umaarufu ndiyo kipimo cha mafanikio.