Jumatatu , 9th Mar , 2026

Iran imerusha makombora yake ya kwanza kuelekea Israeli leo Jumatatu March 09,2026 tangu kuteuliwa kwa Kiongozi Mkuu mpya wa Jamhuri ya Kiislamu, Ayatollah Seyyed Mojtaba Khamenei.

Iran imerusha makombora yake ya kwanza kuelekea Israeli leo Jumatatu March 09,2026 tangu kuteuliwa kwa Kiongozi Mkuu mpya wa Jamhuri ya Kiislamu, Ayatollah Seyyed Mojtaba Khamenei.

Kituo cha utangazaji cha Serikali ya Iran IRIB kimesema kwamba Iran imefyatua wimbi la kwanza la makombora chini ya Ayatollah Mojtaba Khamenei kuelekea maeneo yaliyokaliwa ambapo imechapisha picha ya kombora lenye kauli mbiu "Kwa Amri Yako, Sayyid Mojtaba”.

Wakati haya yakijiri, Waziri Mkuu wa Qatar na Waziri wa Mambo ya nje, Mohammed bin Abdulrahman Al Thani ametoa wito wa kupunguzwa kwa kiwango cha vita vya Iran ambapo akiongea na Sky News amesema hawakutarajia mashambulizi ya jirani yao Iran dhidi ya nchi za Ghuba.

Wakati huohuo shambulizi la droni lililofanywa na Iran nchini Bahrain limewajeruhi Raia 32 katika kisiwa cha Sitre.