Ijumaa , 25th Jul , 2025

Ikiwa tetesi za uhamisho wa mshambuliaji wa Newcastle United, Alexander Isak, kuelekea Liverpool zitathibitika, basi staa huyo kutoka Sweden ataingia moja kwa moja kwenye orodha ya wachezaji wanaolipwa vizuri zaidi katika kikosi cha The Reds.

Kama ataingia kwenye kikosi cha Liverpool, Isak atakuwa analipwa takriban milioni 780 za Kitanzania kwa wiki, akiwazidi mastaa wengi wa Ulaya kwa kipato. Mshahara huu utamweka nyuma ya Mohamed Salah na Virgil Van Dijk tu, ambao kila mmoja analipwa zaidi ya bilioni 1 kwa wiki.

Wachambuzi wanasema Liverpool wangefanya dili kubwa kwa kumsajili Isak kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kufunga, umri wake mdogo, na uthabiti wake ndani ya EPL. Lakini pia, mshahara wake mkubwa unaashiria matarajio makubwa kutoka kwa kocha na mashabiki.