Alhamisi , 26th Feb , 2026

Kesi ya kupinga uteuzi iliyoundwa kwaajili ya kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea nchini Oktoba 29.2025 na siku zilizofuata, inayoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman imeendelea tena leo, Alhamisi Februari 26.2026, Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Da

Kesi ya kupinga uteuzi iliyoundwa kwaajili ya kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea nchini Oktoba 29.2025 na siku zilizofuata, inayoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman imeendelea tena leo, Alhamisi Februari 26.2026, Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam mbele ya Jaji Awamu Mbagwa

Katika kesi hiyo iliyofunguliwa na Watanzania watatu (3) Rosemary Mwakitwange, Deogratias Mahinyila na Edward Heche, waleta maombi wanadai kwamba uteuzi wa Tume hiyo una dosari za msingi, kutokana na kile walichoeleza kuwa kuna uvunjwaji wa sheria pia kukiukwa kwa misingi ya haki ya asili, matumizi mabaya ya mamlaka na nia ovu (mala fide)

Kesi hiyo ambayo leo imekuja kwaajili ya kusikilizwa na Mahakama baada ya kusikiliza inatarajiwa kutoa uamuzi wake Machi 06.2026, waleta maombi hao ambao wawili kati yao ni Mawakili wa Mahakama Kuu wameainisha masuala kadhaa wanayodai kuwa yanafanya kuwa uundaji wa tume hiyo ugubikwe na ukiukwaji wa sheria, moja wapo ni lile wanalodai kwamba Rais aliunda 'Tume huru ya uchunguzi, chombo ambacho kinadaiwa hakijatambuliwa wala kuelezwa katika sheria ya Tume za Uchunguzi inayotumika

Waombaji wanadai pia kwamba uteuzi huo haukutangazwa kwenye Gazeti la Serikali, na kwamba sharti la lazima la kubainisha kwa uwazi madhumuni ya tume hiyo halikuzingatiwa pia

Hoja nyingine iliyoibuliwa inahusu upendeleo na uundaji wa Tume kukosa mantiki, hapa suala lililosisitizwa na waleta maombi ni kwamba wajumbe wa tume hiyo ni wastaafu wa serikali au Mihimili mingine ya Dola lakini karibu wote wamewahi kuteuliwa na Rais, jambo linalowafanya kuwa na mgongano wa kimasilahi, hivyo waleta maombi wanaona kwamba suala hilo litachochea wao kukosa uwezo wa kuchunguza matendo ya watumishi wa umma wa sasa au waliopita, ikiwemo mamlaka iliyowateua.