Jumapili , 6th Jul , 2025

Baada ya Real Madrid kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali katika michuano ya Klabu ya dunia kwa magoli 3-2 dhidi ya Borussia Dortmund huku wakiwa pungufu baada Dean Huijsen kutolewa nje kwa kadi nyekundu, rasmi sasa Los Blancos watakutana na PSG katika hatua hiyo.

Half finalist CWC 2025

Paris Saint German wamefuzu kwa kuitoa Bayern Munich kwa idadi ya magoli 2-0 ndani ya dakika 90 huku PSG wakicheza pungufu baada nyota wao wawili Willian Pacho na Theo Hernández wakotolewa kwa kadi nyekundu na wanatarajia kuukosa mchezo wa nusu fainali utakaopigwa Julai 09 majira ya Saa 4:00 Usiku huko nchini Marekani.

Mchezo mwingine wa nusu fainali utawakutanisha Chelsea dhidi ya Fluminense ya Brazil Julai 08 Saa 4:00 Usiku. The Blues ambao ni mabingwa wa Kombe hili la dunia kwa Klabu mwaka 2021 walipoifunga Palmeiras kwa magoli 2-1, wanatabiriwa kufika fainali pia msimu huu.