Alhamisi , 10th Jul , 2025

Nyota wa Real Madrid Jude Bellingham atakaa nje kwa kipindi cha miezi 3 hadi minne baada ya kukubali kwenda kufanyiwa upasuaji wa bega linalomsumbua kwa muda mrefu.

Jude Bellingham

Muingereza huyo mwenye umri  wa miaka 22 alipata jeraha hilo Novemba 2023 katika msimu wake wa kwanza ndani ya Real Madrid katika mchezo dhidi ya Rayo Vallecano lakini alikuwa akighairisha zoezi hilo ili aisaidie klabu yake na huku akitumia dawa za kumpa nafuu kwa muda.

Licha ya kupambana kuisaidia Los Blancos imalize na mataji msimu huu, jitihda zake zimegonga mwamba baada ya kumaliza msimu wa 2024-2025 bila taji lolote baada ya hapo jana kupoteza nusu fainali ya klabu bingwa ya Dunia 4-0 dhidi ya PSG.