Ijumaa , 29th Jul , 2016

Shule ya Msingi Inyala iliyopo eneo la Iyunga ndani ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya imevamiwa na watu wasiojulikana ambao wanafaya shughuli mbalimbali zikiwemo za kilimo kwa mdai ya kutolipwa fidia tangu wamepisha eneo hilo kwa ujenzi wa Shul

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Prof. Joyce Ndalichako.

Mwenyekiti wa Kamati ya Shule hiyo,Mwajuma Tindwa, yenye shule karibu ya 1800 amesema kuwa kama serikali haitaingilia kati suala hilo huenda shule hiyo ikapoteza hadhi yake.

Bi. Tindwa amesema kuwa kwa mujibu wa hati za makibidhiano za eneo hilo na Wakazi kwamba lilitolewa bure na wazazi hao kwa ajili ya ujenzi wa shule ili kuondoa adha ya watoto kusafiri umbali mrefu kwenda mashuleni lakini sasa wamegeuka na kudai fidia.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo ya Inyara, Mwalimu Irene Itunga amesema kuwa tangu kuzuka kwa mgogoro huo na wananchi shule hiyo imekwama kimaendeleo

Nao baadhi ya Wanafunzi wa Shule hiyo wamesema kuwa tatizo kubwa la kutoendelea kwa shule hiyo ambako kunawaathiri zaidi wako kutokana na wazazi hao kuwasumbua walimu pindi wanapoingia madarasani.