Alhamisi , 28th Mei , 2015

Mawakala wa zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura wametakiwa kuzingatia taratibu na sheria zilizowekwa na tume ya uchaguzi juu ya kujari muda wa kujiandikisha.

Mmoja ya Wananchi wa Iringa akijiandikisha katika hatu za mwisho za zoezi hilo lililokamilika jana

Hatua hiyo imekuja baada mawakala wa kata ya kihesa katika kituo cha shule ya wasichana iliyopo manispaa ya Iringa maeneo ya kichangani kukiuka taratibu zilizopangwa juu ya muda wa kufunga zoezi la uandikishaji.

Diwani kata ya gangilonga kupitia chama cha mapinduzi ccm Nicolina Lulandala ambaye diye diwani wa eneo hilo akizungumzia tukio hilo amesema kuwa ni jambo la kusikitisha na limemshitua.

Nae wakala wa kituo hicho kupitia chama cha demokrasia na maendeleo chadema Gama Msigwa amesema hali hiyo imejitokeza kutokana na kuwa watu walikuwa kwenye foleni na walipewa ridhaa ya kuendelea na afisa mtendaji.

Hata hivyo ameeleza kuwa walishindwa kuzuia kuendelea kwa zoezi hilo la uandikishaji kutokana na kuwa wao hawaluhusiwi kushika vifaa vya kujiandikishia.

zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linatarajiwa kukamilika tarehe 31 mwezi huu katika mkoa wa iringa.