Alhamisi , 24th Jul , 2025

Kuelekea michuano ya CHAN 2024 itakayofanyika katika Nchi za Tanzania, Kenya na Uganda mwezi Agosti, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi amesema kuwa Tanzania haitokuwa msindikizaji katika michuano hii ambayo Tanzania watakuwa mwenyeji 

Profesa Palamagamba Kabudi

''Na sisi Tanzani hatujaingia katika mashindano haya kuwa wasindikizaji tumeingia katika mashindano haya tukijua tutakuwa washindi. Lakini pia tutawadhihirishia tarehe 02 ni jinsi gani Tanzania inaouwezo mkubwa wa kuandaa ufunguzi wa mashindano haya.''

''Tanzania imepata nafasi ya kuandaa mchezo wa ufunguzi si kwa bahati mbaya bali imetokana na hamasa kubwa ya michezo iliyopo nchini na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania katika kuboresha miundombinu ya michezo.

Kama wote mnavyofahamu Tanzania tumeweza kuingia katika aina ya saba za mashindano yanayosimamiwa na CAF, ndio imefanya Tanzania kuwa na vigezo kufanya mechi ya ufunguzi pamoja na uzoefu kuliko wenzet wote''-Prof. Kabudi