Jumapili , 6th Jul , 2025

Nahodha wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo hakuwepo kwenye mazishi ya Diogo Jota  na ndugu yake Andre Silva yaliyoongozwa na  Mchungaji Jose Manuel Macedo katika kanisa katoliki la Igreja Matriz de Dgondomar yaliyofanyika leo Julai 5 huko Gondomar karibu na Porto nchini Ureno.

Cristiano Ronaldo and Diogo Jota

Mazishi hayo Wachezaji wa Liverpool wakiongozwa na nahodha Virgil van Dijk, pamoja na wachezaji wenzao wa timu ya taifa ya Ureno na wachezaji wengine  kutoka mataifa mbalimbali walifunga safari hadi Ureno kushiriki ibada ya mwisho ya mazishi ya mshambuliaji huyo wa Liverpool kufuatia kifo cha kusikitisha katika ajali ya gari kilichotokea Julai 3 nchini Uhispania.

Ruben Neves ambaye alicheza na Jota Wolves alikuwa ni moja wa watu waliosaidia kubeba jeneza la rafiki yake kanisani baada ya kuwasili kutoka Marekani ambapo jana alicheza robo fainali ya kombe la Dunia la klabu

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali kutoka nchini Ureno zinaripoti kuwa Ronaldo hajaenda katika ibada hiyo ya mazishi kwasababu kuonekana kwake katika mji huo mdogo wa Ureno kungeweza kusababisha msongamano na kuzuia ibada hiyo isifanyike kwa utulivu