Jumamosi , 8th Nov , 2014

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara inakabiliwa na upungufu mkubwa wa Dawa na vifaa tiba , hali ambayo imelalamikiwa vikali na wagonjwa na ndugu wanaowauguza katika hospitali hiyo.

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara inakabiliwa na upungufu mkubwa wa Dawa na vifaa tiba , hali ambayo imelalamikiwa vikali na wagonjwa na ndugu wanaowauguza katika hospitali hiyo.

Wakizungumza katika Mahojiano Maalumu na EATV katika hospitali hiyo baadhi ya wagonjwa na ndugu zao wamesema ukosefu wa dawa na vifaa tiba umezorotesha kwa kiasi kikubwa huduma katika hospitali hiyo.

Wamesema Baada ya wagonjwa kupokelewa na kupata Huduma za uchunguzi wamekuwa wanalazimika kununua dawa hizo nje ya hospitali kitendo ambacho wamesema kimekuwa kikiwasababishia usumbufu mkubwa.

Baadhi ya Madaktari wa Hospitali hiyo waliozungumza ya EATV Sharti la kutotajwa majina kwa madai kuwa siyo wasemaji wa suala hilo , wamethibitisha upungufu huo unao ikabili hospitali hiyo .

Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt IRAGI NGERAGEZA, alipo tafutwa kwa simu kuzungumzia malalamiko hayo ya wagonjwa, mara zote imekuwa ikiita Bila majibu na juhudi za kumtafuta zinaendelea.