Rwanda imekuwa Nchi ya Kwanza barani Afrika kwa watengeneza maudhui wa nchini humo wa mtandao TikTok kuweza kupata pesa moja kwa moja kutokana na maudhi wanayotengeza kwenye mtandao huo.
Haya yanajiri kutokana na rufaa ya umma iliyotolewa wakati wa Baraza la 20 la Kitaifa la Umushyikirano, ambapo watengeneza maudhui wa jukwaa hilo walitoa wito kwa Rais wa nchi hiyo Paul Kagame kusaidia kufungua fursa za mapato moja kwa moja kutoka kwenye mitandao hiyo inayolipa watengeneza maudhui.
Kwa muda mrefu sasa, watengeneza maudhui wa TikTok waliopo Afrika wamekuwa wakipata mapato kwenye jukwaa hilo kupitia ushirikiano na chapa mbalimbali, na zana zingine za uchumaji wa mapato kama vile ushirikiano wa wasanii wa muziki pamoja na kupokea zawadi kutoka kwa wafuasi wanaowafuatilia kwenye mtandao huo.


