
Ruben Amorim - Kocha wa Manchester United
Amorim licha ya kutumia pauni milioni 200 kwenye safu ya ushambuliaji msimu huu, lakini kuruhusu bao kupitia kona limekuwa tatizo kwa United kuliko timu nyingine yoyote katika misimu miwili iliyopita. Manchester Utd ndiyo timu iliyoruhusu magoli mengi zaidi kwa njia ya kona (magoli 23) kwenye Premier League tangu kuanza kwa msimu wa 2023-24.
Kinyume chake, katika kipindi hicho, Arsenal wamefunga magoli 31 ikiwa ni tofauti ya magoli 11 dhidi ya Liverpool ambao wamefunga magoli 20. United walimaliza nafasi ya 15 msimu uliopita sawa na mwaka 1974.
Kocha Amorim, hapo jana kilikuwa kipigo chake cha 15 katika mechi 28 za Premier League huku akitoa sare michezo 6 na kushinda michezo 7 pekee akiwa ndio Kocha wa kwanza kufikisha vipigo 15 vya haraka zaidi katika ligi kuu tangu Paul Hart apoteze michezo 15 katika mechi 27 kama kocha wa Portsmouth mwaka 2009, miaka 16 iliyopita.