Huu ni mwanzo bora wa ligi ya kikapu Marekani NBA tangu msimu wa 2015-16 klabu ya Golden State Warriors iliyocheza michezo 24 mfululizo kwenye msimu huo.Donovan Mitchell amekuwa kwenye kiwango bora sana msimu kwa Cavaliers kamaliza mchezo wa jana akiwa amefunga alama 36 na Wachezaji wengine watano wamefikisha alama zaidi ya kumi mchezo wa jana huku ikitoka nyuma kwa alama 9 robo ya tatu na kushinda mchezo huo.
Sababu mbalimbali zimetajwa juu ya uamuzi uliochukuliwa na Uongozi wa timu hiyo kuhamia uwanja wa KMC Complex ikiwemo picha za vidio ambazo hazina uthibitisho kama kweli zinaihusu klabu hiyo zikionyesha mabomba ya sindano uwanjani Azam Complex ikisemekana Wachezaji wake wanaongeza nguvu kwa kuchoma sindano.
Msimamo wa Ligi Kuu nchini Italia Serie A baada ya michezo 12 kuchezwa.
Ushindi wa goli nne kwa sifuri dhidi Osasuna mchezo uliopigwa uwanja wa Santiago Bernabéu Stadium siku ya Jumamosi ya Novemba 9 mchezo huo ulitamatika huku kukiwa na majeruhi wapya kwa kikosi cha mabingwa watetezi wa La liga, Eder Militao atakaa nje ya uwanja miezi 9 baada ya kuumia goti, Rodrygo Goes na Lucas Vazquez wote walipata majeraha kwenye mchezo huo.
Kikosi cha Liverpool msimu 2024-25 kinapewa nafasi ya kuwa mabingwa wa Ligi kuu Uingereza EPL msimu huu.
Yanga itashuka tena dimbani baada ya lenda ya FIFA kukabiliana na Al Hilal katika mchezo wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika mchezo utakaochezwa Novemba 26 2024.Baada ya kupokea kipigo dhidi ya Tabora United kuna taarifa nyingi zilienea kwenye vijiwe vya mpira na mitando ya kijamii kuhusiana na Kocha wa timu hiyo kuwekwa kitimoto na Uongozi wa kikosi cha Wananchi.
Kipigo cha jana kwa Wajangwani kimekuwa cha pili mfululizo baada ya kuruhusu kufungwa goli 1-0 dhidi ya Azam wiki iliyopita. Hii inakuwa mara ya kwanza Yanga SC kupoteza michezo miwili mfululizo tangu mwaka 2020.
Tchakei alionesha kiwango kizuri chenye mwendelezo kwa mwezi Oktoba akiwashinda Lusajo Mwaikenda wa Azam FC na Pacome Zouzoua wa Yanga, alioingia nao fainali katika mchakato wa tuzo za mwezi uliofanywa na Kamati ya tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa mwaka wa 2027 yanatarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza ukanda wa Afrika ya Mashariki kwa ushirikiano nchi tatu Tanzania, Kenya na Uganda ambazo ndizo zitakuwa nchi wenyejiwa mashindano hayo.
Nyota huyo wa zamani wa K.R.C. Genk ya Ubelgiji, TP Mazembe ya Congo DR na Aston Villa ya England kumbukumbu nzuri ya maisha yake ni kufunga goli dhidi ya Manchester City mahasimu wa United kwenye mchezo wa fainali ya kombe la Carabao mwaka 2020.
Takwimu za mechi mbili walizokutana zinaonyesha timu ya Wananchi imeshinda michezo yote miwili dhidi ya Wapinzani wao siku ya leo (3-0, 1-0) Tabora United kutokea Tabora ambayo inashika nafasi ya 10 ikiwa imevuna alama 14 msimu huu.
Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kinashika nafasi ya tatu msimamo wa ligi kuu TPL kikiwa na alama 22 nyuma ya Singida Black Stars yenye alama 23 Yanga SC ikiwa kileleni mwa msimamo ikiwa na alama 24.
Real Madrid inashika nafasi ya pili msimamo wa ligi kuu nchini Hispania ikijikusanyia alama 24 nyuma ya Barcelona iliyoko kileleni na alama zake 33,ligi ya Mabingwa ipo nafasi ya 17 imekusanya alama 6 baada ya kucheza michezo minne.
Nyota huyo wa zamani wa Santos ya Brazil amekitumikia kikosi cha Al-Hilal michezo saba tu tangu ajiunge na timu hiyo kutokea PSG mwaka 2023.