Taarifa kutoka Ikulu iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imsema kuwa uteuzi wa Jaji Lubuva umeanza leo Juni 18, 2018.
Jaji Mstaafu Lubuva anachukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo Bw. Peter Ngubullu.
Jaji Mstaafu Lubuva alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) 2015.







