Kituo cha Polisi cha Bunju A leo kimechomwa moto na wananchi kufuatia vurugu za wananchi hao zilizosababishwa na ajali ya gari eneo la Bunju shule iliyosababisha kifo cha mtoto Tabia Omari aliyekuwa akisoma kwenye shule ya msingi ya Bunju A alipokuwa akielekea shuleni mapema leo asubuhi.
Wananchi hao walichoma kituo hicho kutokana na hasira za kuondolewa kwa wanafunzi na wananchi waliofunga barabara katika eneo la ajali baada ya kusababisha foleni na kuzuia magari yaliyokuwa yakipita katika barabara ya Bagamoyo katika eneo hilo.
Katika eneo hilo pia wanachi walifanya matukio mengine ya kulenga polisi kwa mawe na kubomoa vioo vya magari yaliyokuwa katika eneo hilo kabla ya jeshi la polisi kuongeza nguvu katika eneo hilo na kuanza kuwatawanya wananchi kwa mabomu.
Tukio hilo lilimlazimu mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadik pamoja na Kamanda wa polisi mkoa wa Dar es salaam ACP Camilius Wambura wafike kujionea athari hiyo na kuelezea tukio hilo kwa namna ya kuhuzunika na yaliyotokea.