Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
Rais Kikwete amesema hayo jana wakati wa sherehe za uzinduzi wa mtambo wa kuzalisha umeme wa kutumia gesi wa Kinyerezi Dar es salaam ambapo utazalisha megawati 150 za nishati hiyo.
Aidha Dkt .Kikwete ameongeza kuwa watendaji wa TANESCO kuongeza kasi ya uzalishaji umeme ili kupunguza malalamiko ya watumiaji na kwamba ni muhimu wakafuata sheria za manunuzi ya umma.
Amesema tayari kuna nchi zaidi ya tano Afrika ambazo ziko tayari kununua umeme kutoka Tanzania ikiwemo Msumbiji ambayo inahitaji kuuziwa megawati 300 kutoka nchini.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa TANESCO,Mhandisi Felchesmi Mramba amesema shirika hilo halifanyi hujuma yoyote kama inavyodaiwa na baadhi ya watu na badala yake linafanya kazi kwa kfuata maelekezo ya serikali.