Shai Gilgeous-Alexander
Shai-Alexander rai awa Canada alimaliza mchezo huo uliopigwa Alfajiri ya kuamkia leo akiwa na pointi 35, ambazo zilikuwa nyingi zaidi kwa upande wa timu yake, alivunja rekodi hiyo kwa kufunga mpira wa alama tatu mwanzoni mwa robo ya tatu, baada ya awali kufunga mipira miwili ya adhabu .
Mfululizo huo wa michezo kwa nyota huyo mara nne wa All-Star ulianza tangu mwanzo wa msimu wa NBA wa 2024/25, alipofunga pointi 30 katika ushindi wa pointi 137–114 dhidi ya Trail Blazers Novemba 1,2024 akimuacha mbali Kevin Durant aliyewahi kuwa na rekodi ya kufunga angalau pointi 20 katika michezo 72 mfululizo katika msimu wa 2015/16.
Gilgeous-Alexander anaendelea kuwa katika kiwango cha juu kinachomfanya kuwania tena tuzo ya MVP msimu huu ambapo katika michezo 54 aliyocheza hadi sasa, ana wastani wa alama 31.7 kwa kila mchezo, rebounds 4.5 na pasi za mwisho 6.6 huku akisaidia Oklahoma City Thunder kuongoza ligi ya NBA kwa rekodi bora ya ushindi 51-15 kabla ya mchezo wa Alhamisi

