Rapa huyo wa Marekani amesema angependa kupata nafasi ya kushirikiana na wasanii marehemu Bob Marley na Fela Kuti, ambao wanatajwa kuwa miongoni mwa nguzo muhimu katika historia ya muziki wa Reggae na Afrobeat.
Mbali na wasanii hao wawili waliotangulia mbele ya haki, Ross pia alimtaja nyota wa muziki kutoka Nigeria, Burna Boy, kama mmoja wa wasanii wa sasa ambao angependa kufanya nao kazi.
Rapa huyo alitoa kauli hiyo alipokuwa akifanya mahojiano na CNN Africa, ambapo alizungumzia msukumo wake katika muziki na heshima aliyonayo kwa wasanii waliotoa mchango mkubwa katika muziki wa Afrika.
Kauli ya Rick Ross imeibua mjadala miongoni mwa mashabiki wa muziki, wengi wakieleza kuwa ushirikiano kati yake na Burna Boy unaweza kuleta ladha mpya katika muziki wa kimataifa.



