Jumatano , 4th Mar , 2026

Baada ya Liverpool kupoteza mchezo wao dhidi ya Wolves hapo jana wakipigika 2-1 na kudondosha alama 3 huku wakizidi kujiweka mbali na top four msimu huu, nyota wao wa Zamani Steven Gerrard amewakosoa vikali akidai ni uzembe

Steven Gerrard

Gerrard alilaumu safu ya ulinzi kwa kuruhusu bao la kwanza kutokana na uzembe wa kawaida, na kipa Alisson Becker kwa kuanzisha shambulio la bao la pili. Hakukubaliana na madai ya mashabiki kuhusu faulo dhidi ya Virgil van Dijk kabla ya bao la kwanza, akisisitiza kuwa Van Dijk alipaswa kuwa imara zaidi.

Pia, Gerrard amemtaka kocha Arne Slot kumpa mshambuliaji chipukizi Rio Ngumoha nafasi ya kuanza mechi, akimkataa Gakpo kwa kudai Ngumoha anaweza kufanya vizuri zaidi yake

Msimu huu, Liverpool wamepoteza michezo mitano kutokana na mabao ya dakika za mwisho, hali inayowapa presha kubwa katika mbio za kumaliza ndani ya tano bora, huku Chelsea wakiwa na nafasi ya kuipiku timu hiyo endapo watashinda dhidi ya Aston Villa .