Jumatano , 6th Sep , 2023

Wawekezaji wameaswa kuwekeza zaidi nchini Tanzania katika sekta ya Mifugo kutokana na uwepo wa fursa nyingi kwenye sekta hiyo

Wakati majadiliano yakiendelea kuhusu maboresho kwenye sekta ya kilimo na mifugo, Tanzania inaelezwa kuwa na fursa nyingi za uwekezaji kwenye mifugo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega amewataka wawekezaji kuja na kuwekeza katika sekta hiyo hapa nchini.

"Tuna uwepo wa ardhi ya kutosha ya kilimo ambayo utaipata kupitia taasisi zetu za serikali kikiwepo Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC  ambayo inaweza kusaidia uzalishaji wa mbegu za malisho ya mifugo na soko linalopatikana kwa urahisi la mifugo na mazao ya mifugo nchini Tanzania yenye idadi ya watu milioni 61, soko la kikanda katika EAC na SADC na Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA) lenye watu zaidi ya bilioni 1.4." - Waziri Abdallah Ulega

Katika hatua nyingine kumekuwa na mjadala pia kuhusu usalama wa chakula na maswala ya Jinsia  Africa  na hapa Mama Mariam Mwinyi Mke wa Rais wa Zanzibar anaeleza jambo hilo linavyofanyiwa kazi visiwani zanzibar hususani kwenye zao la mwani

"Visiwani Zanzibar wanawake wengi wanajishuhulisha zaidi katika zao la mwani na pia kwa kiasi kikubwa wanahakikisha usalama wa chakula unakuwepo" - Mariam Mwinyi, Mke wa Rais wa Zanzibar
Pamoja na hayo mawaziri wa Afya wamejadili maswala ya lishe na kuangalia namna gani lishe bora inaweza kuwafikia wananchi wa bara hili.