
Afisa Habari wa Simba Hajji Manara amesema, wamewaacha wachezaji hao kutokana na mapendekezo ya benchi la ufundi katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo.
Manara amesema, haina maana kuwa kila mchezaji anayeachwa na timu hafanyi vizuri bali hiyo inatokana na mapendekezo ya kocha anahitaji kitu gani kifanyike ili aweze kuboresha zaidi kikosi chake.
Kwa upande mwingine Manara amesema, uongozi wa klabu hiyo umekubaliana na ombi la aliyekuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo Suleiman Matola kuomba kuachana na klabu hiyo.