Wawili washikiliwa tukio la mlipuko wa bomu Arusha
Jeshi la Polisi nchini Tanzania linawashikilia watu wawili, kuhusiana na mlipuko uliotokea katika mgahawa karibu na viwanja vya Gymkhana na Mahakama Kuu Jijini Arusha jana usiku ambapo watu wanane wamejeruhiwa vibaya huku mmoja akiwa mahututi.

