Upinzani wadai Zanzibar inapunjwa misaada ya nje
Kambi ya upinzani bungeni imesema mapato ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yanayotokana na misaada na mikopo ya wahisani wa nje, Zanzibar hupewa asilimia ndogo ya mapato hayo kutokana na asilimia kubwa kutumika Tanzania Bara.