Nyalandu aivunja Idara ya Wanyamapori
Waziri wa maliasili na utalii nchini Tanzania Lazaro Nyalandu, ametangaza kuivunja idara ya wanyamapori na kuunda mamlaka ya wanyamapori, kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yake kiasi cha kusababisha matukio ya ujangili na uwindaji haramu.

