Kinondoni wakumbwa na hofu homa ya dengue
Wakazi wa Kinondoni B jijini Dar es salaam nchini Tanzania, wameelezea kukumbwa na hofu ya kuugua ugonjwa wa Dengue kutokana na uwepo wa maji yaliyotuama na kuzunguka nyumba katika maeneo wanayoishi hali inayosababishwa na hali duni ya miundombinu.