Ijumaa , 11th Jul , 2014

Baada ya kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki mjini Mombasa nchini Kenya, Mwimbaji Anto NeoSoul anaendelea na ziara yake ya muziki ya Afrika Mashariki ambapo hivi sasa anajiandaa kutua nchini Tanzania.

Mwanamuziki Anto NeoSoul wa nchini Kenya

Mkali huyo wa kibao maarufu cha Chips Funga ambaye yupo katika ziara hiyo kubwa itakayomchukua muda wa miezi mitatu, ameelezea kuwa atafanya onesho lake jijini Dar es Salaam, mjini Arusha pamoja na mikoa mingine nchini Tanzania.

Anto NeoSoul amesema kuwa lengo zima la ziara hiyo Afrika Mashariki ni maalum kwa ajili ya kuitangaza albamu yake mpya aliyoibatiza jina 'Starborn'.