Tanzania yatakiwa kukabiliana na dawa za kulevya
Shirika la Kimataifa la Madaktari wa ulimwengu limeiomba serikali ya Tanzania pamoja na jamii kwa ujumla kuweka nguvu zaidi katika kutoa huduma kwa waathirika wa madawa ya kulevya nchini na kuacha kuwaadhibu watumiaji wa dawa hizo.

