Alhamisi , 26th Jun , 2014

Shirika la Kimataifa la Madaktari wa ulimwengu limeiomba serikali ya Tanzania pamoja na jamii kwa ujumla kuweka nguvu zaidi katika kutoa huduma kwa waathirika wa madawa ya kulevya nchini na kuacha kuwaadhibu watumiaji wa dawa hizo.

Waziri wa nchi, ofisi ya waziri mkuu, Sera, uratibu na bunge, William Lukuvi.

Akiongea jijini Dar es Salaam, meneja wa mafunzo wa shirika la kimataifa la madaktari wa ulimwengu maarufu kwa jina la Medicenes du Monde wakati dunia ikiadhimisha siku ya kupingana na madawa ya Kulevya hii leo, Bi. Damali Lukas amesema mpaka sasa wameshawahudumia waathirika wa dawa hizo elfu tisa tangu kunzishwa kwake nchini Tanzania .

Wakati huo huo, Mkuu wa Kitengo cha matibabu kwa waathirika wa dawa za kulevya katika hospitali ya Mwananyamala Bi. Pili Said amesema kuwa nguvu kazi kubwa ya taifa inapotea kutokana na vijana kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya ambapo mpaka sasa katika hospitali hiyo takribani waathirika 660 wa dawa wanapatiwa matibabu huku akiainisha aina ya dawa hizo za kulevya.