Timu shiriki Afrika kuanza safari Agosti 30
Timu sita shiriki za michuano ya All Africa Games zinatarajiwa kuanza kuondoka nchini Agosti 30 mwaka huu kuelekea nchini Congo Brazzaville kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba nne mwaka huu.

