Rais Magufuli awalilia waliofariki ajalini Kilolo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza kufuatia ajali ya basi kugongana na lori, na kusababisha vifo vya watu 12, na wengine 15 kujeruhiwa