Mwenyekiti wa DRFA Almasi Kasongo
Mhinzi amesema amesikia kupitia vyombo vya habari kuwa amefungiwa miaka miwili kutojishugulisha na maswala ya mpira wa miguu,kwa sababu alikiuka kanuni za uchaguzi.
Mhinzi amehoji kanuni gani aliyoivunja na kama anafungiwa basi aelezwe kwa barua,kuliko kudharirishwa kwenye vyombo vya habari.
Mhinzi amesema DRFA inataka kuihujumu TEFA na kudidimiza soka la Temeke, kwa kuwa kuna watu wanawatumia kuinyemelea TEFA.
Mhinzi aliyeshinda uchaguzi kwa mizengwe mwezi Novemba mwaka uliopita,amesema atatoa msimamo wake kuhusu TEFA na maamuzi ya DRFA,pale atakapopewa barua rasmi ya kufungiwa.
Mwenyekiti wa DRFA Almasi Kasongo ilikataa kuutambua uongozi wa TEFA kwa kuwa walifanya uchaguzi wakati kesi ipo mahakamani baada ya baadhi ya wanachama kufungua kesi wakiipinga kamati ya uchaguzi ya TEFA.
Baadhi ya wanachama walioongea na chombo chetu wamesema kinachotafutwa na viongozi wa DRFA ni mradi wa maduka yaliyojengwa na TEFA, ambapo mradi huo unawaaumiza viongozi wa DRFA wakitamani kupitisha watu wao kwenye chama hicho ili waingize mkono wa kula.


