Waziri Mkuu afungua duka la MSD wilayani Ruangwa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amefungua duka la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) katika Hospitali ya wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi ambalo litakuwa na uwezo wa kuhudumia hospitali 524 katika mikoa ya Lindi, Mtwara na wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
