Dkt. Mollel amtumbua Mganga Mkuu Arusha na wenzake
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel ameagiza kuondolewa kwa safi ya uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru inayoongozwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Shafii Msechu ikiwa ni sehemu ya maboresho katika afya.

